Pages

Sunday, 5 April 2015

NIMEIKUMBUKA NIGERIA YA AKINA TARIBO WEST,JAY JAY OKOCHA ,BABAYARO WALIKUWA "SIMBA WASIOFUGIKA" KWELI



Nigeria moja kati ya timu zilizopata kupendwa sana kabla haijapoteza mwelekeo siku za hivi karibuni
Nikukumbushe kikosi cha Nigeria ambacho kilishiriki na kutwaa ubingwa wa michuano ya Olimpiki, Atalanta, Marekani, 1994 kilijumuhisha wachezaji waliokuja kutamba barani Ulaya kama, Sunday Oliseh, Austin Jay Jay Okocha, Finidi George, Tijani Babangida, Celestine Babayaro, Godwin Okpara, Victor Ikpeba, Nwanko Kanu wakali wengine wengi. Nigeria iliweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka barani Afrika kutwaa taji medali ya dhahabu katika michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka minne wakati wa majira ya kiangazi.

Chini ya kocha, Mjerumani, ‘ Super Eagle’ iliifunga Brazil katika hatua ya nusu fainali wakati huo kikosi cha Mario Zagallo kilikuwa na wakali kama, Roberto Carlos, Ronaldo De Lima, Rivaldo Fereirra, Cafu na asilimia kubwa ya wachezaji ambao waliifikisha Brazil katika fainali ya kombe la dunia, 1998. Nigeria ilisukwa kizalendo licha ya asilimia kubwa ya wachezaji kucheza Ulaya. ‘ Moyo wa safu ya ulinzi’ alikuwa, Taribo West, hakika kilikuwa kizazi cha dhahabu kilichokosa bahati kutoka bara la Afrika.

Nigeria ile haikuwahi kutwaa taji lolote ndani ya bara la Afrika’, kitendo cha kupoteza mchezo wa fainali mbele ya Cameroon katika ardhi ya nyumbani katika michuano ya AFCON, 2000 kiliwaumiza mashabiki wengi wa soka duniani ambao walikuwa wakiifuatilia kwa karibu timu hiyo kutoka Ukanda wa Afrika. Kandanda safi muda wote wa michuano, mkusanyiko wa vipaji bora vya soka vyenye uzalendo ndani ya uwanja vilivutia kutazama ‘ Tai wa Kijani’ wakiuzungusha mpira kila sehemu ya uwanja.

Nigeria ilipotea baada ya miaka minne na hapo, ‘ Simba wasioshindika’ wakawavutia wapenzi wa soka. Ushindi wa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki, Sydney, Australia, 2000 ilikuja baada ya Cameroon kutwaa ubingwa wa AFCON, 2000 kwa kuichapa, Nigeria mwezi, April kwa changamoto ya mikwaju ya penalti. Cameroon walikuwa wakitawala mechi kutokana na kuwa na wachezaji wa ‘ nguvu-nguvu’, Cameroon ilikuwa timu ambayo mataifa mengi ya ulaya ‘ hawakukuitaka’. Cameron ni mabingwa wa Olimpiki, 2000 tena waliinyamazisha timu iliyotawala dunia kwa miaka minne iliyopita ya Hispania.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates