Real madrid leo wameshusha kipigo cha mbwa mwizi kwaGranada, ambao hawajawahi kushinda Uwanjani Santiago Bernabeu tangu Januari 1974 waliposhinda 1-0 na tangu wakati huo wamecheza Mechi 20, Leo tena wameendeleza uteja kwa kubamizwa Bao 9-1 kwenye Mechi ya La Liga na Real Madrid huku Cristiano Ronaldo akipiga Bao 5.
Hadi Mapumziko Real walikuwa mbele kwa Bao za Garreth Bale na Hetitriki ya Ronaldo.
Kipindi cha Pili Karim Benzema alifunga Bao 2, Ronaldo kuongeza 2 na Bao moja Granada kujifunga wenyewe kupitia Mainz.
Ushindi huu, ambao ni mkubwa kwa Real tangu 1967, umeifanya Real, walio Nafasi ya PIli kwenye La Liga, wawakaribie Vinara Barcelona wakiwa Pointi 1 nyuma yao.
Pia kwenye vita ya Pichichi, Tuzo ya Mfungaji Bora wa La Liga, Ronaldo ambae alikuwa nyuma ya Lionel Messi kwa Bao moja, sasa yuko mbele kwa Bao 4 akiwa na Jumla ya Mabao 36.
0 comments:
Post a Comment