Pages

Monday, 6 April 2015

YANGA SASA KUCHEZA NA TIMU YA ZAMANI YA OKWI NI ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA 17-19 MWEZI HUU

Baada ya kumsubiri mpinzani wa Yanga katika hatua inayofuata hatimaye imefahamika sasa wakutana na Etoile du Sahel ya Tunisia baada ya waarabu hao kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Benfica de Luanda ya Angola katika mechi yao ya marudiano ya Kombe la Shirikisho.
Etoile imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya mchezo wa kwanza nyumbani kushinda bao 1-0 na sasa watavaana na Yanga waliosonga mbele dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe ambao jana waliwacharaza bao 1-0.
Kipigo hicho cha ugenini hakikuizuia Yanga kusonga mbele kwani ilikuwa na hazina ya ushindi wa mabao 5-1 yaliyopatikana katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.
Yanga imefuzu katika hatua ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho ikiwa na timu nyingine 15.
Mechi ya mko
ndo wa kwanza ya Yanga na Etoile itachezwa kati ya April 17-19 jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana mjini Tunisia wiki mbili baadaye ambapo mshindi atasubiri kucheza mchujo wa mwisho dhidi ya timu zitakazoangukia pua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye Juni tayari kwa ajili ya kutinga hatua ya makundi kuvuna mamilioni ya CAF.
Aidha TP Mazembe ya DRC imesonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya leo kushinda nyumbani 3-1 na kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 ugenini.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates