Simba sc leo wamepata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya kagera sugar katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliomalizika katika uwanja wa kambarage shinyanga.
Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kunako dakika ya 49 kipindi cha pili kupitia kwa Ramadhan Singano kabla ya Kagera kusawazisha kupitia kwa Rashid Mandawa.Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib aliipachikia timu hiyo goli la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penati, Kufatia ushindi huo Simba inakuwa imefikisha pointi 35 baada ya kucheza michezo 21.
0 comments:
Post a Comment