Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City Jana walichapwa 2-1 na Crystal Palace huko Selhurst Park na kuvurugiwa kabisa utetezi wa Taji lao.
Kipigo hiki ni cha 4 mfulilizo cha Ugenini na kimewaacha wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wana Mechi 1 mkononi na pia kubakishwa Nafasi ya wakiwa pia nyuma ya Arsenal na Manchester United.
Bao zilizowaua City hapo Jana zilifungwa na Gllenn Murray Dakika ya 34 na Jason Puncheon Dakika ya 48 wakati Bao la City lilifungwa Dakika ya 78 na Yaya Toure.
Ushindi huu umewarusha Crystal Palace hadi Nafasi ya 11.
Mechi inayofuata kwa City ni Jumapili ijayo huko Old Trafford kwenye Dabi ya Manchester dhidi ya Man United.
0 comments:
Post a Comment