Pages

Friday, 10 April 2015

MATUSI YAMPONZA IBRAHIMOVIC AFUNGIWA MECHI NNE



Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic amefungiwa kucheza mechi nne za ligi kuu ya Ufaransa baada ya kunaswa na picha za televisheni akitukana.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Sweden alikasirika na kuwashutumu waamuzi na pia kutukana baada ya timu yake kupoteza 3-2 dhidi ya Bordeaux mwezi uliopita. Ibrahimovic, 33, baadaye aliomba radhi na kusema matamshi yake "hayakuwa yamelenga Ufaransa au wananchi wake"
.
Atakosa mechi nne kati ya saba zilizosalia za ligi. Kamati ya nidhamu ilisema adhabu hiyo imezingatia "aina ya kosa na uzito wa matamshi yake".
Ibrahimovic pia atakosa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Champions League dhidi ya Barcelona kufuatia kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea. Hata hivyo ataweza kucheza mechi ya fainali ya kombe la ligi siku ya Jumamosi dhidi ya Bastia.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates