Pages

Wednesday, 1 April 2015

MECHI ZA KIRAFIKI ZA KIMATAIFA: HISPANIA YATANDIKWA 2-0 NA UHOLANZI, UINGEREZA NAO WATOA SARE NA ITALY

Spain wameshindwa kulipa kisasi cha kutandikwa 5-1 na Netherlands Mwaka Jana kwenye Fainali za Kombe la Dunia baada Usiku huu kuchapwa tena 2-0 ndani ya Amsterdam ArenA.

Hadi mapumziko Netherlands walikuwa mbele kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Stefan De Vrij, Dakika ya 13, na Davy Klaassen, Dakika ya 16.
Italy na England Usiku wa jana wametoka Sare ya 1-1 kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa Juventus Stadium Jijini Turin.
Italy walikwenda Haftaimu wakiwa mbele kwa Bao la Dakika ya 29 la Straika anaechezea huko England kwenye Klabu ya Southampton, Graziano Pelle, aliefunga kwa Kichwa kutoka krosi ya Giorgo Chiellini alieunasa mpira wa kona.
Kipindi cha Pili Dakika ya 79, Andros Townsend, alieingizwa Dakika 10 kabla, aliisawazishia England kwa shuti la Mita 25 ambalo lilimshinda Kipa Mkongwe Buffon.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates