Pages

Wednesday, 1 April 2015

SASA SIMBA KUGAWA MAGARI NA SIMU KALI KWA WACHEZAJI WANAOJITUMA

Kampuni ya EAG Group Limited, imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu Simba kwa ajili ya kuitafutia mipango thabiti ya kuiendesha timu hiyo kuhakikisha inapiga hatua katika maendeleo yake.

EAG Group iliingia mkataba na timu hiyo leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Simba, Evans Aveva alisema kuwa kwa kumpitia udhamini wa kampuni hiyo wameandaa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wao kuhakikisha wanajituma uwanjani.
Aveva alizitaja tuzo hizo ni ya mchezaji bora wa mwaka atakayepewa gari jipya, mchezaji kijana mwenye kipaji atkayepewa milioni 5 na mchezaji mwenye nidhamu atakayeramba milioni moja.

Pia, wachezaji hao wote kila mmoja atapewa zawadi ya simu aina ya Huawei yenye thamani ya shilingi milioni moja ambao nao wameingia kwenye udhamini huo.
“Lengo tunataka kuona timu yetu inapiga hatua katika soka ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika Mashariki na Kati na ndiyo tumetoa zawadi hizo kwa ajili ya kuwapa morali wachezaji wetu kupitia Kampuni ya EAG Group Limited na Huawei,” alisema Aveva.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates