Bao za Raheem Sterling na Joe Allen za kila Kipindi Jana huko Anfield ziliwapa ushindi wa Bao 2-0 Liverpool walipocheza na Newcastle katika Mechi pekee ya Ligi Kuu England.
Bao hizo zilifungwaa katika Dakika za 9 na Sterling na Dakika ya ya na Allen.
Newcastle walibaki mtu 10 kuanzia Dakika ya 83 baada ya Moussa Sisoko kupewa Kadi ya Njano ya Pili na hivyo kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Ushindi huu wa Liverpool umewapandisha hadi Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 4 Man City.
Timu 4 za juu kwenye Msimamo wa Ligi ndizo zitacheza Mashindano makubwa Barani Ulaya Msimu ujao ya UEFA
Msimamo Timu za Juu:
1. Chelsea Mechi 31 Pointi 73
2. Arsenal Mechi 32 Pointi 66
3. Man United Mechi 32 Pointi 65
4. Man City Mechi 32 Pointi 61
5. Liverpool Mechi 32 Pointi 57
6. Southampton Mechi 32 Pointi 56
7. Tottenham Mechi 32 Pointi 54
0 comments:
Post a Comment