Pages

Thursday, 9 April 2015

SIMBA KUCHEZA NA TOTO AFRICAN KESHO TIMU IPO MWANZA KUTEMBELEA MARSH ACADEMY

Kikosi cha mabingwa wa kombe la mapinduzi Simba SC kiko jijini Mwanza kwa ziara ya kukitembelea kituo cha Marsh Academy sambamba na kuwapa ladha ya ligi ku timu ya Toto African iliyorejea ligi kuu ya Tanzania bara mwezi uliopita.

Kesho kikosi cha Simba SC kitatembelea kituo cha Marsh Academy, ambacho kiliasisiwa na kocha wa zamani wa timu za taifa ya Tanzania,
Sylvester Marsh.
 ambaye alifariki mwezi uliopita marehemu
Ziara hiyo ya simba SC katika kituo hicho ni kwa ajili ya kumuenzi marehemu Sylveser Marsh aliyeifanyia mambo makubwa soka la Tanzania.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wanakwenda kwenye kituo hicho kuonyesha wanamuenzi Marsh lakini kuonyesha Simba inajali ukuzwaji wa wachezaji vijana.

"Kuhusiana na vijana, Simba ni timu inayojali vijana na ndiyo timu inaongoza kutumia vijana hata katika kikosi chake kikubwa.

"Hivyo tutafika pale kutembelea kituo hicho, tutatoa rambirambi na kumuenzi Marsh ambaye alitoa mchango mkubwa kwa vijana wakati wa uhai wake," alisema Manara.

Baada ya ziara hiyo hapo kesho Simba SC siku ya jumamosi wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Toto African, ikiwa ni sehemu ya kuwakaribisha katika ligi kuu ya vodacom.
Manara alisema kuwa Simba juma mosi watawakaribisha Toto Afrika katika ligi kuu ya vodacom kabla ya jumapili kuanza safari ya kurejea Dar es salaam na jumatano kuanza safari yakwenda Mbeya kuwakabili Mbeya city katika uwanja wa Sokoine.
Simba SC wapo Mwanza baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Kagera sugar uliochezwa katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga siku ya jumatatu ya wiki hii.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates