Pages

Thursday, 9 April 2015

HABARI ZA USAJILI ULAYA: NYOTA WATATU WA LIVERPOOL KUTUA MANCHESTER CITY YUMO STERLING PIA



Manchester City imemuorodhesha Phillipe Coutinho kama mchezaji wa tatu wanayepanga kumnunua kutoka kwa mahasimu wao Liverpool.
Timu hiyo tajiri inapanga kutumia mamilioni ya fedha kuwanunua wachezaji wapya mwishoni mwa msimu huu kufuatia matokeo mabaya.
Mabingwa hao wanapanga kukibadilisha kikosi hicho hatua ambayo huenda ikawakosesha taji lolote.

Mwenyekiti Khaldoon Al- Mubarak ameandika majina ya baadhi ya wachezaji wakiwemo nyota wa England Raheem Sterling na Jordan Henderson.
Imebainika kuwa kilabu hiyo pia inapanga kumnunua mchezaji wa Brazil Coutinho.

Inadaiwa kuwa wakuu wa kilabu hiyo wanaamini Coutinho anaweza kuhamishwa hadi katika uwanja wa Etihad kwa kitita sha pauni millioni 20 iwapo Liverpool itashindwa kuorodheshwa miongoni mwa timu nne bora zitakazofuzu kucheza katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Habari hizo huenda zikamshtua Brendan Rodgers ambaye anawaona wachezaji wake wakiwindwa na kilabu pinzani.
Rodgers angependa sana kuwazuia wachezaji wake katika uwanja wa Anfield lakini pia anajua kwamba hawezi kushindana na mfuku mzito wa mmiliki wa kilabu hiyo Sheikh Mansour
.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates