FIFA Leo hii imetoa Listi ya Ubora Duniani kwa Nchi na Mabingwa wa Dunia Germany wameendelea kuwa juu wakifuatiwa na Argentina huku Tanzania ikishuka Nafasi 7 na kushika Nafasi ya 107.
Nchi ya juu kabisa kwa Afrika bado ni Algeria lakini imeporomoka Nafasi 3 na sasa ipo ya 21 ikifuatiwa na Ivory Coast ambayo pia imeshuka Nafasi 3 na ipo ya 23.
Nchi mpya kwenye 10 Bora ni Switzerland na Spain wakati France na Italy zimetoka huko.
Nayo Belgium imepanda Nafasi 1 na ni wa 3 baada ya kuchukua nafasi ya Colombia huku Brazil wakipanda moja wakiwa Nafasi ya 5.
England nao wanaisogelea 10 Bora baada kupanda Nafasi 3 na kushika Nafasi ya 14.
Listi nyingine ya Ubora itatolewa hapo Mei 7.
TIMU 10 BORA DUNIANI:
20 BORA:
1 Germany
2 Argentina
3 Belgium
4 Colombia
5 Brazil
6 Netherlands
7 Portugal
8 Uruguay
9 Switzerland
10 Spain
0 comments:
Post a Comment