Mbio za Ubingwa wa La Liga huko Spain ziliendelea huko Spain kwa Vinara Barcelona kushinda na kubaki Pointi 4 mbele ya Real Madrid ambao nao Jana walishinda huku Staa wao, Cristiano Ronaldo, akipiga Bao 1 na kufikisha Bao 300 kwa Timu hiyo.
Huko Nou Camp, Barcelona iliichapa UD Almeria Bao 4-0 kwa Bao za Lionel Messi, Luis Suarez Bao 2 na Marc Batra.
Ushindi huu umewafanya Barca waendelee kuongoza Ligi wakiwa Pointi 4 mbele ya Real.
Nao Real Madrid, wakicheza Ugenini huko Estadio Teresa Rivero Jijini Madrid waliichapa Rayo Vallecano Bao 2-0 kwa Bao za Cristiano Ronaldo na James Rodriguez.
Bao la Ronaldo limemfanya azidi kuongoza katika Ufungaji Bora wa La Liga akiwa na Mabao 37 na kufuatiwa na Messi mwenye Bao 33 lakini pia umemfanya afikishe Bao 300 kwa Real na kumweka Nafasi ya 3 nyuma ya Alfredo Di Stefano, Bao 308, na Raul Bao 323 katika Historia ya Ufungaji Bora wa Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment