Philippe Coutinho, Staa wa Brazil, Jana Uwanjani Ewood Park aliipeleka Liverpool Nusu Fainali ya FA CUP alipofunga Bao pekee na la ushindi katika Dakikia ya 70 kwenye Mechi ya Marudiano walipoichapa Blackburn Rovers, Timu ya Daraja la Championship, 1-0
Mwezi Jana Timu hizi zilitoka 0-0 huko Anfield na kulazimisha Marudiano haya.
Kwenye Nusu Fainali, ambayo itachezwa Wembley Jijini London, Liverpool watacheza na ASton Villa wakati NUsu Fainali nyingine ni Reading v Arsenal.
NUSU FAINALI ZOTE ZITACHEZWA WEMBLEY
Jumamosi Aprili 18
1920 Reading v Arsenal
Jumapili Aprili 19
1700 Aston Villa v Liverpool
0 comments:
Post a Comment