Yanga ambao ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Ilionyesha dhamiri ya dhati kuweza kuibuka na ushindi leo baada ya kuanza kwa mashambulizi ya nguvu ambayo yalizaa goli la kwanza kwa yanga likifungwa kwa Ustadi na Mshambuliaji aliyetemwa na Simba Amiss Tambwe kwa kichwa goli ambalo lilizaa mengine matatu kwa tambwe na kumfanya kuondoka na mpira katika mchezo huo kwa kufunga magoli manne peke yake.
Winga na Mshambuliaji aliye katika hali nzuri ya kufunga hivi sasa Simon Msuva yeye alitupia bao 2 peke yake wakati Salum Telela na Mliberia Kpah Sherman nao walitupia bao moja kila mmoja na kukamilisha ushindi wa bao 8-0 ushindi ambao pengine utavunja rekodi katika ligi kuu.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa wamezidi kujichimbia kileleni mwa ligi kuu kwa kufikisha pointi 43 na mechi ijayo Yanga itamenyana na Mbeya City Jijini Dar Jumapili hii.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Wagonga nyindo wa jijini Mbeya, Mbeya city hii leo wameikomalia Azam Fc na kufanikwa kwenda nayo sare ya kufungana goli 1-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex.
.
Katika mchezo wa leo ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko wakiwa bado hawajafanikiwa kuona nyavu za wapinzani wao.
Azam FC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Kipre Bolue katika dakika ya 61 kabla ya Mbeya city kusawazisha kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Rafael Daudi na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana goli moja moja.
Mchezo huo ni mchezo wa pili mful;ulioz katika uwanja wa Azam complex Mbeya city wanapata sare dhidi ya Azam FC, baada ya msimu uliopita kufanikiwa kupata sare ya kufungana goli 3-3
0 comments:
Post a Comment