Arsenal Jana Usiku iliichapa AS Monaco 2-0 kwao Stade Louis II Jijini
Monaco ambako hawajafungwa tangu 2005 lakini wametupwa nje ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI kwa Bao za Ugenini na hii ni mara ya 5 mfululizo kwa
Arsenal kushindwa kutinga Robo Fainali.
Arsenal walifungwa kwao Emiratez Bao 3-1 na matokeo ya Jana kufanya Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili kuwa 3-3 na AS Monaco kutinga Robo Fainali kwa Ubora wa Bao za Ugenini.
Hii ni mara ya kwanza kwa AS Monaco kufika Robo Fainali tangu 2004.
Bao za Arsenal hiyo Jana zilifungwa na Olivier Giroid Dakika ya 36 na Aaron Ramsey, alietoka Benchi, na kufunga Dakika ya 79.
Katika Mechi nyingine iliyochezwa Jana huko Vicente Calderon Jijini Madrid, Wenyeji Atletico Madrid wametinga Robo Fainali kwa Mikwaju ya Penati 3-2 baada ya kufungana Mabao na Bayer Leverkusen 1-1 kwa Mechi mbili.
Leverkusen walishinda kwao Germany 1-0 na Jana Atletico kushinda 1-0 kwa Bao la Dakika ya 27 la Mario Suarez na kudumu hadi Dakika 90 kwisha na hivyo Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30 bila kubadilika.
Ndipo ikaja Mikwaju ya Penati 5 na Atletico kushinda Penati 3- 2 huku Antoine Griezman, Mario Suarez na Fernando Torres wakifunga na Raul na Koke wakikosa kwa upande wa Atletico wakati Leverkusen wafungaji ni Rolfes na Castro na Calhanoglu, Toprat na Stefan Kiesling wakikosa.
Atletico, ambao Msimu uliopita walifungwa Fainali ya Mashindano haya na Real Madrid, sasa wanaingia Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI itakayofanyika Ijumaa pamoja na A S Monaco, Real Madrid, FC Porto, Bayern Munich na Paris Saint-Germain.
Timu nyingine mbili za mwisho zitakazotinga Robo Fainali zitajulijana Leo baada ya Mechi kati ya Barcelona na Man City na ile kati ya Borussia Dortmund na Juventus.

0 comments:
Post a Comment