Pages

Sunday, 15 March 2015

MCHEZO WA YANGA NA PLATINUM HAUTAONYESHWA KWENYE LUNINGA NAO AZAM WATUMA SALAM ZA KHERI

Vinara wa ligi kuu ya vodacom Yanga wametangaza mchezo wao kombe la shirikisho dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe utakao chezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam hautoonyeshwa na kituo chochote cha luniga.

Mkuu wa kitengo cha habari wa yanga Jerry Muro amesema kuwa mchezo wao  hautoonyeshwa, hivyo mashabiki wanatakiwa wafike katika uwanja wa Taifa, na wasitegemee kuona mchezo huo kupitia luninga zao za nyumbani.
Muro aliwataka watanzania wote wajitokeze kwa wingi katika uwanja wa Taifa na kuipa sapoti timu ya yanga, ambao ndio wawakishi pekee wa Tanzania aliyesalia katika michuano ya kimataifa.
Muro alisema kuwa ni wakati wa kujivua usimba, uyanga na uwanjani  kwa mashabiki wote kuwa wa moja katika mchezo huo dhidi ya FC Platinum, ambayo imewatoa SOFAPAKA ya Kenya kwa kuwafunga nyumbani na ugeninin jumla ya magoli 4-2. 

AZAM WAMEITAKIA HERI YANGA NA WAMEANDIKA KWENYE ACCOUNT YAO YA FACEBOOK
Azam FC inaitakia ushindi wa magoli mengi klabu ya Yanga kwenye mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Platinum Stars ya Zimbabwe. Ushindi wa Yanga leo na hatimaye kuitoa Platinum utakuwa ni ushindi wa Tanzania kwani Yanga ndiyo klabu pekee iliyosalia kwenye mashindano ya kimataifa.
Tunawaomba mashabiki wetu popote mlipo hasa mtakaoenda uwanjani, kuishangilia na kuiombea dua Yanga ili iweze kupata ushindi.
Tukiwa kwenye ligi ya VPL sisi ni washindani, lakini kwenye mashindano ya kimataifa Yanga wanawakilisha taifa letu.
Mungu ibariki Yanga, Mungu ibariki Tanzania
Share:

2 comments:

  1. Mlisema na kweli dua zetu zimesikika. Yanga imetimiza kile mashabiki wataka. wadau wote wa mpira mtakubaliana nami kuwa yanga walicheza. na wametupa matokeo mazuri, wamefuta kilio cha kufungwa na simba. Mungu ibariki yanga, Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Mlisema na kweli dua zetu zimesikika. Yanga imetimiza kile mashabiki wataka. wadau wote wa mpira mtakubaliana nami kuwa yanga walicheza. na wametupa matokeo mazuri, wamefuta kilio cha kufungwa na simba. Mungu ibariki yanga, Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates