Simba imeendeleza ushindi baada ya kuichapa Ndanda FC kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Hata hivyo, Simba walionekana kutulia na kupiga pasi za haraka na fupifupi na dakika ya 16 wakapata bao la pili Ramadhani Sinagano ‘Messi’ baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Ndanda, Saleh Malande.
Said Ndemla akaongeza bao la tatu katika dakika ya 32 baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Ibrahim Ajibu.
Ajibu huyohuyo alishindwa kuifungia Simba bao la nyongeza baada ya kukosa penalti iliyotolewa baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa katika eneo la hatari.
Kipindi cha pili kilionekana cha ushindani mkubwa lakini bado Simba waliafanikiwa kulinda mabao yao matatu na Ndanda kutoka hawana kitu.
Simba ilionyesha kiwango cha juu katika mchezo huo na kufanikiwa ushindi wa mabao hayo matatu.
Ilianza kalamu yake ya mabao kupitia kwa Jonas Mkude katika dakika ya nane tu na bao hilo likawafanya Ndanda kuamka na kushambulia kwa kasi.Hata hivyo, Simba walionekana kutulia na kupiga pasi za haraka na fupifupi na dakika ya 16 wakapata bao la pili Ramadhani Sinagano ‘Messi’ baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Ndanda, Saleh Malande.
Said Ndemla akaongeza bao la tatu katika dakika ya 32 baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Ibrahim Ajibu.
Ajibu huyohuyo alishindwa kuifungia Simba bao la nyongeza baada ya kukosa penalti iliyotolewa baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa katika eneo la hatari.
Kipindi cha pili kilionekana cha ushindani mkubwa lakini bado Simba waliafanikiwa kulinda mabao yao matatu na Ndanda kutoka hawana kitu.
0 comments:
Post a Comment