Pages

Wednesday, 22 April 2015

REAL WAICHAPA 1-0 ATLETICO NAO JUVE WATOA SARE NA MONACO SASA TIMU 4 NUSU FAINALI DROO KUPANGWA IJUMAA

Javier Hernandez 'Chicharito', Mchezaji wa Mkopo kutoka Manchester United Jana aliwapeleka Real Madrid Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kufunga Bao pekee na la ushindi katika Dakika ya 88 kwenye Mechi ya Marudiano ya Robo Fainali iliyochezwa Uwanjani Santiago Bernabeu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Real, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Mashindano haya, kuifunga Atletico katika Mechi 8 zilizochezwa tangu Mwezi Mei Mwaka Jana walipoitwanga Atletico Bao 4-1 huko Lisbon na kutwaa Kombe hili.
Bao hilo la ushindi lilitokana na ustadi wa Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo ambae alisonga mbele na Mpira na kumpa Pasi murua Chicharito aliemalizia vizuri na kuipa Real ushindi wa Bao 1-0.
Katika Dakika ya 75 Arda Turan wa Atletico alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Wiki iliyopita, huko Nyumbani kwa Atletico Uwanja wa Vicente Calderon, Timu hizi zilitoka 0-0.
**************
Juventus wametinga Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya kwanza tangu 2003 baada ya Jana kutoka Sare ya 0-0 Ugenini huko Stade Louis II, Monte Carlo na AS Monaco.
Wiki iliyopita, Juve waliifunga AS Monaco Goli 1-0 katik Mechi ya kwanza Nyumbani kwao Turin, Italy kwa Bao lililofungwa kwa Penati ya Arturo Vidal.
*************


Kwenye Nusu Fainali, Juve wanaungana na Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich na Mechi zake zitapangwa Ijumaa Aprili 24 huko Nyon, Uswisi kwenye Droo maalum ambayo Timu yeyote inaweza kupangiwa Timu nyingine yeyote bila kujali Utaifa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates