Pages

Thursday, 21 May 2015

ANGALIA TETESI MBALIMBALI ZA USAJILI ULAYA STORI KUBWA RAHEEM STERLING KUTUA MANCHESTER CITY AU BAYERN

RAHEEM STERLING AWANIWA NA MAN CITY,ARSENAL NA BAYERN MUNICH
Huku kukiwa na ripoti kuwa Mchezaji Bora Kijana wa Liverpool kwa Msimu huu, Raheem Sterling, akiwa njiani kuiambia rasmi Klabu yake anataka kuhama na Chelsea, Manchester City, Arsenal na Bayern Munich zikimlilia, Mahasimu wakubwa wa Liverpool, Manchester United, nao wamejitumbukiza kumuwania.
Licha ya kuwepo nafasi duni kwa Liverpool kukubali kuwauzia wapinzani wao wakubwa Man United Staa wao, imeripotiwa kuwa Mawakala toka Old Trafford wamepiga hodi kuulizia kuhusu uwezekano wa kumnunua Sterling.
Inatarajiwa Ijumaa Jioni, Raheem Sterling na Mwakilishi wake, Aidy Ward, watakutana na Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers pamoja na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Ian Ayre, na hapo ndipo rasmi Sterling atatamka kutaka kuihama Liverpool Msimu huu.
Ripoti pia zimedai kuwa Liverpool imeijulisha Man United kuwa Sterling si biashara kwao kwa Dau lolote. 
Lakini Wachambuzi wanahisi mlengwa mkuu wa Sterling ni Man City ambao wako tayari kumlipa Winga huyo Chipukizi wa England mwenye Miaka 21 Mshahara wa Pauni 150,000 kwa Wiki badala ya Pauni 100,000 aliyopewa Ofa mpya kwenye Mkataba mpya na Liverpool ambao ameukataa.
*****************************
XAVI KUONDOKA BARCELONA
Kiungo wa Barcelona Xavi yupo tayari kutangaza kuwa anaondoka Barcelona kwenda kujiunga klabu ya nchini Qatari Al Sadd kwa mkataba wa miaka mitatu, anasema wakala wake.
Xavi, 35, amekuwa na miamba hiyo ya La Liga kwa miaka 17, akishinda mataji manane ya La Liga, mataji matatu ya Champions League na mataji mengine kadhaa.
Mchezo wake wa mwisho wa ligi kukipiga kwa mabingwa wapya wa La Liga utakuwa dhidi ya Deportivo La Coruna Jumamosi ijayo.
Barcelona bado ina nafasi ya kutwaa Champions League na Copa del Rey.
Kwa mujibu wa wakala wake, Ivan Corretja, Xavi anaweza pia kuwa balozi wa Kombe la Dunia mwaka 2022 ambalo litafanyika nchini humo kabla ya kuanza harakati zake za kuwa kocha.
Xavi ameichezea timu ya taifa ya Uhispania mara 133 - ikiwa ni rekodi - na alikuwa sehemu muhimu ya ushindi wa Kombe la Dunia mwaka 2010 na ubingwa wa Ulaya mwaka 2008 na 2012.
******************************
Fowadi wa Real Madrid Gareth Bale, 25, anataka kubaki kwenye klabu hiyo yaLa Liga, akifikisha mwisho matumaini ya Manchester United kumtumia kama dili la kumnasa kupitia mlinda mlango David De Gea, 24. (Mirror)
Bale aliambiwa kubaki klabu hapo ikiwa ni mipango ya muda mrefu ya Real kwenye mkutano na wakurugenzi wa klabu. (Sun)
****************************
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anafikiria kutoa ofa kwa mshambuliaji wa Aston Villa kutoka Ubelgiji Christian Benteke, 24, ambaye ana thamani ya paundi 30m. (Daily Mirror)
Mlinzi wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels, 26 - ambaye anawindwa kwa muda mrefu na klabu ya Manchester United - ameamua kukataa kuhamia England. (Bild - in German)
*************************
Manchester City na Chelsea zinamuwania kiungo wa Barcelona Alex Song, 27. Song amekuwa kwa mkopo kwenye klabu ya West Ham. (Mail)
************************
City pia wanamuwinda mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino, 21. (Daily Star)
Wakati huo huo, Yaya Toure, 32, anaonekana na kila dalili za kuondoka Etihad, ambapo Inter Milan wanakaribia kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast. (The Times)
****************************
Liverpool itatangaza kuwa winga Jordon Ibe, 19, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya paundi 35,000 kwa wiki. (Sun)

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates