Jana huko Britannia Stadium Liverpool waliaaga Msimu wa Ligi Kuu England kwa kichapo hicho cha Bao 6 na pia kumuaga Kepteni wao Steven Gerrard ambae anaondoka kwenda kumalizia Soka lake huko Marekani.
Rodgers amekiri kuwa yuko kwenye presha kubwa baada ya kushinda Mechi 2 tu katika 9 zilizopita na kumaliza Nafasi ya 6 kwenye Ligi ikimaanisha Msimu ujao watacheza UEFA EUROPA LIGI.
Pia Rodgers amekiri ni fedheha kwa Timu yao kupigwa Bao 6 kitu ambacho hakijatokea kwao kwa Miaka 52 na kuwaomba radhi Mashabiki wao.
Katika Mechi hiyo Brendan Rodgers alimpiga benchi Staa wao Raheem Sterling ambae amegoma kusaini Mkataba mpya na kung'ang'ania kuhama.
Hadi Mapumziko Liverpool ilikuwa nyuma kwa Bao 5-0 zilizofungwa ndani ya Dakika 23 na Mame Biram Diouf, Bao 2, Jonathan Walters, Charlie Adam na Steven N'Zonzi.
Bao pekee la Liverpool lilifungwa na Steven Gerrard katika Kipindi cha Pili ambacho pia Stoke walipiga Bao lao la 6 kupitia Peter Crouch.
0 comments:
Post a Comment