Klabu ya Ligi Kuu England Sunderland hivi karibuni imetembelea Tanzania ikiongozwa na Mkuu wao wa Kuendeleza Soka Kimataifa, Graham Robinson, ambae alizuru Migodi Miwili inayomilikiwa na Acacia Mining ili kutoa Mafunzo ya Soka kwa Jamii zinazoishi jirani na Migodi hiyo.
Acacia Mining plc, ndiyo inayomiliki Migodi ya Dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.
Ziara hiyo ya Graham ni Mradi wa pamoja wa Klabu ya Sunderland na Acacia Mining ili kutoa Mafunzo ya Soka na Ukocha kwa Timu za Migodi hiyo na Makocha wao.
Mafunzo hayo yalifanyika Bulyanhulu Mine School yakijumuisha Makocha wa Timu ya Acacia pamoja na Makocha kutoka Vijiji jirani.
Akiongelea kuhusu Mafunzo hayo, Graham alisema: "Tulitoa mafunzo ya vitendo kadhaa na Makocha walishiriki kikamilifu na kuuliza maswali mengi."
"Soka ya Jamii ndio chanzo cha Wachezaji wengi na kupitia Washirika wetu Barani Afrika tuna Miradi ya muda mrefu na tunasifika kwa kuwekeza katika Programu za Elimu katika Jamii."
0 comments:
Post a Comment