Liverpool, wakiwa kwao Anfield, walitangulia kufunga katika Dakika ya 19 kwa Bao la la Philippe Coutninho na QPR kusawazisha Dakika ya 73 Mfungaji akiwa Leroy Fer.
Liverpool walipewa Penati Dakika ya 79 na Gerrard kuikosa na kisha Dakika ya 82 QPR kubaki Mtu 10 baada ya Nedum Ohuoha kupewa Kadi za Njano 2 ndani ya Dakika 3 tu na kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 87, Gerrard akafunga Bao la ushindi kwa Liverpool na kuweka hai matumaini yao finyu ya kufuzu 4 Bora wakiwa Nafasi ya 5 Pointi 4 nyuma ya Man United wenye Mechi 1 mkononi huku Liverpool wakibakiza Mechi 3.
MANCHESTER UNITED WAKUBALI KICHAPO
Kwenye Mechi waliyotawala kila kitu na pia kupata Penati, Manchester United wamejikuta wakichapwa Bao 1-0 kwao Old Trafford na West Bromwich Albion na kufungua matumaini makubwa kwa Liverpool na Tottenham kuweza kuwaporomosha kutoka Nafasi ya 4 ya Ligi Kuu England.
Bao la ushindi la WBA lilifungwa Dakika ya 64 baada Frikiki ya Chris Brunt kumbabatiza Jonas Olsson na kutinga.
Man United walipata Penati Dakika ya 74 na Robin van Persie kupiga na Kipa Myhill kuokoa.
Matokeo haya yamewaacha Man United, ambao sasa wameshushiwa kipigo chao cha 3 mfululizo, Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 4 juu ya Liverpool huku wote wakibakisha Mechi 3.
0 comments:
Post a Comment