Baada ya Burnley kuwa Timu ya kwanza kuporomoka Daraja kutoka Ligi Kuu England Msimu huu, Leo hii huko Etihad Manchester City ambao wamevuliwa Ubingwa na Chelsea Wiki iliyopita wameibamiza Queens Park Rangers na kuishusha Daraja huku wakibakiza Mechi 2.
Usnindi huu pia umewafanya City wajizatiti Nafasi ya Pili na kujihakikishia kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
MAGOLI:
-Sergio Aguero Dakika ya 4
-Aleksandar Kolarov 32
-Sergio Aguero 50
-Sergio Aguero 65 [Penati]
-James Milner 70
-David Silva 87
Straika wa City anaetoka Argentina, Sergio Aguero, aliepiga Bao 3 amezidi kuongoza kwa Ufungaji Bora wa Ligi Kuu England akiwa na Bao 25.
0 comments:
Post a Comment