Pages

Saturday, 2 May 2015

MKE WA RIO FREDINAND AFARIKI DUNIA KUTOKANA NA KANSA

Mke wa Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Nahodha wa England Rio Ferdinand amefariki Dunia kutokana na Ugonjwa wa Kansa.
Rio, mwenye Miaka 36 na ambae sasa anachezea QPR, ametoa taarifa ya Kifo cha Mkewe kilichotokea kwenye Hospitali Jijini London.
Mkewe Rio, Rebecca Ellison, Miaka 34, alipatwa na tatizo la Kansa ya Ziwa.

Rio na Rebecca walioana Mwaka 2009 baada ya kuwa wakiishi pamoja na wana Watoto Watatu.
Klabu ya QPR imetangaza kuwa Kikosi chao Leo kitavaa Vitambaa Vyeusi Mikononi wakati wa Mechi yao ya Ligi Kuu England huko Anfield dhidi ya Liverpool.
Ferdinand alikulia huko Peckham, London ya Kusini Mashariki na aliichezea England mara 81 na pia kuzichezea Klabu za West Ham United na Leeds United.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates