Wenyeji Chile na Bolivia wametinga Robo Fainali za Copa America baada ya kushinda Mechi zao za mwisho za Kundi A Jana Usiku.
CHILE 5-0 BOLIVIA
Wakicheza Estadio Nacional de Chile Mjini Santiago, Chile waliibamiza Bolivia 5-0 kwa Bao za Charles Aranguiz, Dakika za 3 na 79, Alexis Sanchez, 66, Gary Medel, 86, na Ronald Raldes kujifunga mwenyewe.
Licha ya Bolivia kupata kipigo hicho, wao wamefuzu kutinga Robo Fainali kwa kumaliza Nafasi ya Pili.
Nao Ecuador wametwaa Nafasi ya 3 ya Kundi A baada ya kuichapa Mexico 2-1 na wanangojea Makundi mengine kumaliza Mechi zao na kujua kama wataingia Robo Fainali kwa Tiketi moja kati ya mbili za Mshindi wa Tatu Bora toka Makundi yote Matatu.
MEXICO 1-2 ECOADOR
Bao za Ecuador kwenye Mechi hiyo zilifungwa na Miler Bolanos na Luis Antonio Valencia katika Dakika za 56 na 67 na Mexico kupata Bao lao moja kwa Penati ya Dakika ya 64 iliyopigwa na Raul Jimenez.
Leo zipo Mechi mbili za mwisho za Kundi B ambpao Vigogo Argentina watacheza na Timu Mwalikwa Jamaica na Mabingwa WAtetezi Uruguay kukipiga na Paraguay.
MSIMAMO:
KUNDI A
1 Chile Pointi 7
2 Bolivia 4
3 Ecuador 3
4 Mexico 2
KUNDI B
1 Argentina Pointi 4
2 Paraguay 4
3 Uruguay 3
4 Jamaica 0
KUNDI C
1 Peru Pointi 3
2 Brazil 3
3 Colombia 3
4 Venezuela 3
********************************************
COPA AMERICA MICHEZO YA LEO
Jumamosi Juni 20
KUNDI B Uruguay v Paraguay (Saa 4 Usiku)
KUNDI B Argentina v Jamaica (Saa 6 na Nusu Usiku)
0 comments:
Post a Comment