Pamoja na kikosi cha Ruvu Shooting kushuka daraja, uongozi wa Maafande hao umefunguka kuwa haupo tayari kumpeleka beki wake, George Michael ‘Beki Katili’ katika timu yoyote hata kama ya jeshi kwa sababu bado wana mkataba naye.
Awali iliripotiwa kuwa JKT Ruvu ilipeleka maombi kwa ajili ya kumuomba beki huyo kuongeza nguvu kwenye kikosi chao msimu ujao.
Ofisa habari wa timu hiyo, Masau Bwire alifunguka kuwa beki huyo watashuka naye na hakuna timu ambayo inaruhusiwa kumchukua.
Awali iliripotiwa kuwa JKT Ruvu ilipeleka maombi kwa ajili ya kumuomba beki huyo kuongeza nguvu kwenye kikosi chao msimu ujao.
Ofisa habari wa timu hiyo, Masau Bwire alifunguka kuwa beki huyo watashuka naye na hakuna timu ambayo inaruhusiwa kumchukua.
******************
iungo wa Klabu ya Simba Jonas Mkude anatarajiwa kwenda Afrika Kusini Alhamisi Juni 26 mwaka huu kwa majaribio ya wiki mbili katika Klabu ya Bidvest Wits.Akiongea na tovuti ya Simba, Mkude alisema fursa hii ni adimu na anaamini akifanikiwa ataiwakilisha vyema Simba na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumzia pengo litakaloachwa ikiwa atafanikiwa majaribio alisema “pengo langu linaweza kuzibwa kwani Simba ina wachezaji nyota wanaojituma na wenye uwezo”***********************
Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, Jamal Kisongo amesema hatma ya mshambuliaji huyo kucheza soka la kulipwa Ulaya sasa itasubiri mwakani kutokana na rais na mmiliki wa klabu yake yake TP Mazembe Moise Katumbi kuonesha bado anahitaji huduma yamchezaji huyo hususan katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika.***********************
Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm ametamka kuwa wachezaji wawili wa Ghana wakati wowote wanatarajiwa kutua nchini kujiunga na kikosi hicho kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika, mwakani.
Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kamati yao ya utendaji kuruhusu klabu za ligi kuu kusajili wachezaji saba wa kimataifa.
0 comments:
Post a Comment