Antoine Griezmann alifunga mabao mawili na kuwawezesha Atletico Madrid kuwachapa Marseille 3-0 mjini Lyon, Ufaransa na kushinda Kombe la Europa League mara yao ya tatu katika kipindi cha miaka tisa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alianza kwa kufunga baada ya Andre Zambo Anguissa kutomakinika na mpira dakika ya 21 na kisha akafunga la pili dakika ya 49.
Nahodha wao Gabi alifunga bao la tatu dakika ya 89 na kuwawezesha vijana hao wa Madrid kushinda kombe hilo ambalo pia walilitwaa miaka 2010 na 2012.
Huzuni kubwa kwa Nahodha wa Marseille Dimitri Payet aliyeondoka uwanjani akichechemea kutokana na jeraha baada ya kukaa uwanjani nusu saa pekee, na sasa huenda akakosa kushiriki Kombe la Dunia kitun kilichomfanya Payet kudondosha chozi.
Bila kiungo huo wao, Wafaransa hao waliwatishia Atletico mara moja pekee, mshambuliaji wa zamani wa Fulham Kostas Mitroglou alipogonga mlingoti wa goli kwa mpira wa kichwa.
0 comments:
Post a Comment