Pages

Sunday, 13 May 2018

NGORONGORO HEROES YAAMBULIA KIPIGO BIFU LA KOCHA NA MCHEZAJI MAUMIVU KWA TAIFA

TANZANIA imejiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele katika mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Mali jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Tanzania, Ngorongoro Heroes sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini kuanzia 2-0 Mei 20 mjini Bamako katika mchezo wa marudiano ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Niger mwakani.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Comoro, Soulaimane Ansudane aliyepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera Mmadi Faissoil na Abdoulmadjid Azilani, hadi mapumziko tayari Mali walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Ousmane Diakite alianza kuifungia Mali dakika ya 37 akitumia makosa ya kipa wa Ngorongoro Heroes, Abdultwali Msheri kupiga mpira bila uangalifu, ambao ulinaswa na wapinzani na kufunga.
Wakati Ngorongoro Heroes wanahangaika kutafuta bao la kusawazisha, wakajikuta wakichapwa bao la pili rahisi kwa makosa ya kipa tena, mfungaji Samadiare Dianka kwa shuti la mpira wa adhabu.
Msheri alikwenda kusimama nyuma ya ukuta wa wachezaji wake na kumrahisishia Dianka kazi kwa kuupeleka mpira upande uliokuwa wazi, kushoto kwa mlinda mlango huyo.
Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Paul Peter akaifungia Ngorongoro Heroes bao la kufutia machozi dakika ya 44 akiuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Mali, Youssouf Keita kufuatia shuri la mpira wa adhabu.
Kipindi cha pili mvua iliyoanza kunyesha tangu asubuhi ikaongezeka na ladha ya mpira ikapungua kutokana na uwanja kuwa unateleza na haikuwa ajabu matokeo hayakubadilika.
Kipigo cha leo lawama zinakwenda kwa Kocha Mkuu, Ammy Ninje ambaye  hakumpanga kipa namba moja, Ramadhani Kabwili ambaye alitofautiana naye kabla ya mchezo wa leo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates