Mchezaji wa timu ya KMC ya Jijini Dar es Salaam, Ally Msengi amepata
nafasi ya kufanya majaribio katika moja ya timu kubwa nchini Ufaransa.
Msengi anatarajia kwenda kujiunga na Lille ya nchini Ufaransa kwa ajili ya kufanya majaribio.
Wakala maarufu wa wachezaji, Paul Michell kutoka kampuni ya Siyavuma ya nchini Afrika Kusini amesema tayari kila kitu kwa Msengi kimeenda vizuri.
“Kila kitu kimekwenda vizuri na sasa kuna mambo kadhaa ya kumalizia kabla ya yeye kuanza safari,” alisema.
Wakati akiwa chini ya umri wa miaka 17, Msengi alikuwa nahodha wa Serengeti Boys iliyokuwa inashiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.

0 comments:
Post a Comment