Matumaini ya Arsenal kufuzu kuingia Robo Fainali za UEFA CHAMPINZ LIGI sasa zipo mashakani baada ya kutwanga kwao Emirates Bao 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na AS Monaco ya France ambayo ni Timu ya zamani ya Meneja wa Arsenal Arsene Wenger.
Wegi walidhania Mechi hii ni ubwete kwa Arsenal pale Droo ilipofanyika lakini AS Monaco walikuja mbogo na kudhihirisha udhaifu mkubwa wa Difensi ya Arsenal.
Monaco walitangulia kupata Bao katika Dakika ya 38 kupitia Geoffrey Kondogbia na kisha Straika wa zamani waMahasimu wa Arsenal, Tottenham, na pia Man United, Dimitar Berbatov, akapiga Bao la Pili Dakika ya 53.
Arsenal walikomboa Bao 1 katika Dakika za Majeruhi kupitia Alex Oxlade-Chamberlain lakini muda huo huo Monaco wakaenda 3-1 mbele kwa Bao la Yannick Ferreira Carrasco na kumwacha Arsene Wenger akiugulia kwa uchungu huku Meneja wa Monaco, Leonardo Jardim, akikimbia na kurukaruka kwa furaha.
Timu hizi zitarudiana huko France hapo Machi 17.
Bayer 04 Leverkusen 1 Atletico de Madrid 0
Bayer 04 Leverkusen wakicheza kwao huko Ujerumani wameichapa Atletico de Madrid Bao 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Bao la Dakika ya 57 la Hakan Calhanoglu ndilo limewapa ushindi Bayer Leverkusen dhidi ya Mabingwa wa Spain Atletico Madrid ambao walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada ya
Kiungo wao Tiago kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano 2.
Timu hizi zitarudiana huko Vicente Calderon, Nyumbani kwa Atletico, hapo Machi 17.
0 comments:
Post a Comment