
Azam FC, ambao ndio Mabingwa wa Tanzania Bara, watakuwa huko Khartoum, Sudan kurudiana na El Merreikh katika Mechi ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Yanga, ambao wanacheza Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho, watakuwa huko Gaborone, Botswana kurudiana na BDF XI katika Mechi ya Raundi ya Awali.
Ili kufuzu, Yanga na Azam FC, zote zinatakiwa kuepuka vipigo lakini hata wakifungwa Bao 1-0 si mbaya kwao.
Ikiwa Azam FC watafuzu basi watatinga Raundi ijayo na kukutana na Mshindi kati ya Lydia Ludic B.A. ya Burundi na Kabuscorp do Planca ya Angola ambazo zilitoka 0-0 katika Mechi yao ya kwanza huko Bujumbura.
Kwa Yanga, ikiwa watapita dhidi ya BDF XI, ambayo ni Timu ya Jeshi la Botswana, basi watakutana na Mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimbabwe ambazo katika Mechi yao ya Kwanza huko Nairobi Platinum ilipata ushindi wa Ugenini wa Bao 2-1.
Nazo Klabu za Zanzibar, KMKM na Polisi, zina kibarua kigumu kwelikweli Wikiendi hii huko Visiwani Unguja baada ya wote kucharazwa kisawasawa Ugenini katika Mechi zao za Kwanza.
Kwenye Kombe la Shirikisho, wakicheza Raundi ya Awali, Polisi ilitandikwa Bao 5-0 na CF Mounana huko Nchini Gabon wakati KMKM, ambao wapo CAF CHAMPIONZ LIGI, walipigwa 2-0 na Al Hilal huko Khartoum katika Mechi ya Raundi ya Awali.
0 comments:
Post a Comment