Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 za EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi Usiku kuwania kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Kwa Klabu za Uingereza, Mbali ya Everton waliopata ushindi mnono wa Ugenini Wiki iliyopita walipoichapa BSC Young Boys ya Uswisi Bao 4-1 na hivyo kujiweka nafasi nzuri kufuzu wakicheza Marudiano kwao Goodison Park, Liverpool nao walipata ushindi kiduchu wa Nyumbani wa Bao 1-0 kwa Bao la Penati ‘aliyoiteka’ Mario Balotelli walipocheza na Besiktas na hivyo kujipa matumaini kufuzu huko Uturuki.
Lakini kwa Spurs, na hasa Celtic, kazi ni ngumu baada ya kupata Sare za Magoli Nyumbani kwao na hivyo kuwa na kazi kubwa kwenye Mechi zao za Marudiano za Ugenini ambazo lazima washinde au wapate Sare za Magoli ya zaidi ya ilivyotokea katika Sare za Mechi zao za Kwanza.
Spurs, wakicheza kwao White Hart Lane, walitoka 1-1 na Fiorentina ya Italy katika Mechi ambayo walitangulia kufunga Dakika ya 6 kwa Bao la Roberto Soldado na Fiorentina kusawazisha Dakika ya 36 kwa Bao la Jose Maria Basanta.
Celtic, wakiwa kwao Celtic Park Mjini Glasgow huko Scotland, walitoka 3-3 na Vigogo wa Italy, Inter Milan ambao waliwatangulia 2-0 kwa Bao za mapema za Xherdan Shaqiri na Rodrigo Palacio za Dakika za 4 na 13.
Celtic walisawazisha Bao zote hizo Dakika za 24 na 25 wafungaji wakiwa Armstrong na Campagnaro, aliejifunga mwenyewe, lakini Inter walipiga Bao la 3 Dakika ya 45 kwa Bao la Pili la Rodrigo Palacio na Celtic kunusurika Dakika ya 90 baada ya Guidetti kurudisha.
0 comments:
Post a Comment