Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo Julio leo ameonekana katika mazoezi ya Coastal union, ambayo imemchukuwa kama kocha msaidizi wa timu hiyo, akimsaidia kocha toka Kenya James Nandwi
Julio akizungumza baada ya mazoezi ya coastal union amesema kuwa amekuja kutimiza ahadi aliyoitoa wakati kikosi chake cha Mwadui kilipo cheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal union.
"Wakati tumekuja kwenye mechi ya kirafiki kati ya timu yangu Mwadui FC na coastal union tulikubaliana, nikimaliza tu, mijekuweza kuwasaidia kufikia malengo, sasa nimekuja kufanya lile nililo ahidi kwa sababu mie ni mtu nilikamilika akili na nasema nimukaja kufanya kile tulicho kisudia na sasa na kuendelea coast itatisha," alisema Julio.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao wa coast inasema
"Jamhuri Kihwelo 'Julio' atua Coastal Union Kuongeza Nguvu Katika benchi la Ufundi.
Karibu Sana Julio"
Mchezo wa kwanza kwa Julio katika kiti cha usaidizi ndani ya coastal union ni dhidi ya Mgambo shooting siku ya jumamosi hii (februari 28).
Wednesday, 25 February 2015
Home »
» JAMUHURI KIHWELO JULIO ATUA TANGA KUMSAIDIA NADWI KUINOA COAST UNION








0 comments:
Post a Comment