Pages

Wednesday, 25 February 2015

TIMU YA TAIFA YA KUOGELEA KUSHIRIKI MICHUANO YA KANDA HUKO ANGOLA MWEZI MEI


KOCHA wa timu ya Taifa ya Kuogelea, Alex Mwaipasi amesema Tanzania inatarajiwa kushiriki kwenye mashindano ya Kanda ya Nne yaliyopangwa kufanyika nchini Angola, Mei mwaka huu. 

Mara ya mwisho mashindano hayo kufanyika ilikuwa ni mwaka jana nchini Uganda ambapo Tanzania iliwakilishwa na wachezaji kadhaa waliofanya vizuri wakiwamo Hilal Hilal na Sonia Tomiotto. 


 Mwaipasi alisema katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika mashindano ya mwaka huu, tayari wameshaanza mchakato wa kusaka kikosi bora. 

“Tumeanza mchakato wa kuwatafuta wachezaji bora kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Morogoro na Dar es Salaam na tuna imani mambo yatakuwa mazuri tutakapoanza kambi baadaye,” alisema Mwaipasi. 

Alisema wachezaji hao watafuatiliwa mwenendo wao katika mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mwezi ujao, na mashindano ya wazi ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika Kusini.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates