Huko Ujerumani zipo habari kuwa Uwanja wa Signal Iduna Park na Maeneo
ya jirani yalilazimika kuondolewa Watu baada ya kugundulika Bomu ambalo
halijalipuka.
Bomu hilo lenye uzito wa Ratili 550 inasemekana ni la asili ya Uingereza na Maafisa walikuwa wakiendelea kujaribu kulitegua.
Ugunduzi wa Bomu hilo ulisababisha Mkutano na Wanahabari wa Kocha wa
Borussia Dortmund, Jurgen Klopp, kuhusu Dabi yao ya Jumamosi dhidi ya
Schalke kuahirishwa.
Huko Germany kugundulika kwa Mabomu ambayo hayajalipuka kutoka Vita
Kuu ya Pili Duniani iliyopiganwa kuanzia Mwaka 1939 hadi 1945 ni kitu
cha kawaida kwani Nchi hiyo iliyokuwa ikitawaliwa na Fashisti Hitler
ilikuwa ikivurumishwa na Mabomu kutoka kwa Uingereza na Washirika wake
pamoja na Urusi.
Kwenye Vita hvyo, Mji wa Dortmund uliharibiwa vibaya kwa kuangushiwa Mabomu kutoka kwenye Ndege za Kivita.
Friday, 27 February 2015
Home »
» BOMU LA VITA KUU YA PILI YA DUNIA LAGUNDULIKA KWENYE UWANJA WA BORUSSIA DORTMUND
0 comments:
Post a Comment