Liverpool,
ambao walishinda Mechi yao ya kwanza huko Anfield Wiki iliyopita, Leo
wamechapwa Bao 1-0 na Besiktas huko Uturuki na Mechi kwenda Dakika 30 za
Nyongeza lakini Matokeo yakabaki hivyo hivyo na ikaja Mikwaju ya Penati
5 na Besiktas kushinda 5-4.
Dejan Lovren ndie aliekosa Penati muhimu ya Liverpool.
Nao
Tottenham, wakicheza Ugenini baada ya Sare ya Nyumbani ya 1-1,
walipigwa Bao 2-0 na Fiorentina huko Italy kwa Bao za Kipindi cha Pili
za Mario Gomes na Mchezaji wa Chelsea Mohamed Salah.
Celtic,
wakicheza Ugenini baada ya Sare ya Nyumbani ya 3-3 na Inter Milan,
walitandikwa Bao 1-0 huko San Siro Milan, Italy kwa Bao la Freddy Guarin
la Dakika ya 88.
Everton, ambayo ilipata ushindi mnono wa Ugenini Wiki iliyopita walipoichapa BSC Young Boys ya Uswisi Bao 4-1, Leo huko kwao Goodison Park wameitandika tena Young Boys Bao 3-1.
Bao
za Everton zilifungwa na Romelu Lukaku, Bao 2 moja la Penati, na
jingine la Kevin Mirallas huku Bao la Young Boys likifungwa na Sekoiu
Junior Sanogo.
Nao
Mabingwa Watetezi Sevilla wamesonga baada ya kuifunga Borussia
Mönchengladbach 3-2 huko Germany na hiki ni kipigo cha Pili kwa
Wajerumani hao baada ya pia kuchapwa 1-0 katika Mechi ya Kwanza.
Washindi wa Raundi hii watajua Wapinzani wao Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakati Droo ya Mechi zao itakapofanyika Leo Ijumaa Mchana huko Nyon, Uswisi.
0 comments:
Post a Comment