Mchezaji wa Serbia, Zarko Udovicic, alitishiwa kwa Bastola na
Mashabiki wa Timu yake baada ya kukosa Penati kwenye Mechi ya Ligi Kuu
Nchini humo kati ya Klabu yake Novi Pazar na FK Rad.
Habari hizi zimetangazwa na FIFPro, Chama cha Kutetea Haki za Wachezaji wa Kulipwa Duniani.
Zarko Udovicic, ambae ni Beki, alipaisha Penati yake katika Dakika ya
85 kwenye Mechi ambayo Wapinzani wao FK Rad walishinda Bao 1-0.
Siku mbili baada ya Mechi hiyo Washabiki wa Novi Pazar walitinga
Mazoezini mwa Timu hiyo na kumtishia Mchezaji huyo kwa Bastola
iliyogandamizwa Usoni mwake.
Hivi sasa imedaiwa Zarko Udovicic, mwenye Miaka 27, ameikimbia Klabu hiyo inayocheza Superliga huko Serbia.
Friday, 27 February 2015
Home »
» UMEISIKIA HII YA ZARKO LUDOVICIC MCHEZAJI ALIYETISHIWA BASTOLA BAADA YA KUKOSA PENATI
0 comments:
Post a Comment