Cristiano Ronaldo Jana Usiku alipiga Bao moja na kuipaisha Real Madrid kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Barcelona baada ya kuifunga Ugenini Elche Bao 2-0.
Bao zote za Real zilifungwa Kipindi cha Pili na la kwanza kupitia Karim Benzema na Ronaldo kupiga Bao la Pili kwa Kichwa.
Bao hilo la Ronaldo limemfanya afikishe Bao 290 kwa Real Madrid na kumuweka Nafasi ya 3 katika Ufungaji Bora katika Historia ya Klabu hiyo akiwa Bao 33 nyuma ya Mfungaji Bora Raul mwenye Mabao 323 huku Nafasi ya Pili ikishikwa na Alfredo Di Stefano mwenye Bao 305.
Hapo Jana, Barcelona waliikosa Nafasi ya kuipiku Real uongozi wa La Liga kwa muda baada ya kuchapwa 1-0 na Malaga tena wakiwa kwao Nou Camp.
0 comments:
Post a Comment