Licha ya kukwaruzana mara kwa mara na Maafisa wa Soka wakiwemo Mameneja wa Timu pinzani na pia kudai ipo kampeni chafu dhidi ya Timu yake Chelsea, Mourinho amekiri maisha Jijini London ni murua na burudani.
Ameeleza: “London ni Peponi kwa maisha ya Kijamii. Kwingineko Ulaya, nguvu ya Soka imefanya maisha yetu yawe magumu na misukosuko. Hapa England, mitaani Watu wanakuchukulia kawaida tu. Unaweza kutembea Barabarani, ukaenda kununua vitu Madukani na Familia yako, ukenda Hotelini kwa Chakula bila bughudha!”
Ameongeza: “Maisha ya Kijamii hapa yametulia. Kuna msemo hapa England kwamba mzuka wa Soka huwa ni Dakika 90 tu kwa Wiki na baada ya hapo kila kitu ni poa tu!”
0 comments:
Post a Comment