Pages

Saturday, 21 February 2015

TANZANIA MBABE SOKA LA UFUKWENI YAITANDIKA KENYA 7-6 YASONGA MBELE SASA KUWAWINDA MISRI

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) imepata ushindi wa magoli 7 kwa 6 katika mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, mchezo ulioanza majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Escape One Club Msasani jijini Dar es salaam. 

Hadi mapumziko Kenya walikuwa mbele kwa magoli 3 kwa 2
 

Katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mombasa, timu ya Taifa ya Tanzania iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 3 dhidi ya wenyeji timu ya Taifa ya Kenya na kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.
 . 

Kwa ushindi huo Tanzania inasonga raundi inayofuata ya mashindano hayo kwa uwiano wa magoli 12 kwa 9 ambapo sasa itacheza na timu ya taifa ya Misri
Fainali za Soka la Ufukweni zinatarajiwa kufanayika mapema mwaka huu katika Visiwa vya Shelisheli.
Share:

1 comment:

  1. Juma unajisikiaje siku ukakuta picha zako kwenye blog yangu nimezitumia na sijakupa Acredit? Si vizuri kutumia kazi ya mtu bila kumpa acredit

    ReplyDelete

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates