Pages

Saturday, 28 February 2015

YANGA YAPIGWA 2-1 NA BDF LAKINI YASONGA MBELE SASA YANGA ITACHEZA NA SOFAPAKA AU PLATINUM LEO ZAMU YA AZAM NA KMKM

Huko Gaborone, Botswana hapo Jana, Yanga ilifungwa Bao 2-1 na BDF XI kwenye Mechi ya Pili ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho lakini wamesonga na kutinga Raundi ya Kwanza kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya kushinda Mechi ya Kwanza 2-0 Mjini Dar es Salaa.
Kwenye Mechi ya Jana, Yanga walitangulia Bao 1-0 hadi Mapumziko alilofunga Mrisho Ngassa lakini BDF XI Kipindi cha Pili walifunga Bao 2 na Gemu kwisha 2-1 huku Yanga pa wakiwa Mtu 10 baada ya Danny Mrwanda kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 70.
BDF XI pia walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 21 baada ya Mchezaji wao Mparithe kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Katika Raundi ijayo, Yanga watacheza na Mshindi kati ya Platinum ya Zimbabwe na Sofapaka ya Kenya ambao wanarudiana Wikiendi hii huku Platinum wakiwa washindi wa Bao 2-1 katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Nairobi.
Leo, Timu nyingine mbili za Tanzania, Azam FC na KMKM, zitakuwa Viwanjani kwenye Mechi zao za Pili za Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONS LIGI wakati Polisi ya Zanzibar itacheza Mechi yake ya Pili ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho hapo Jumapili.
Azam FC wanahitaji Sare, au hata kufuungwa Bao 1-0, ili kusonga, Timu za Zanzibar, KMKM na Polisi, zinahitaji ushindi mzito ili kupindua matokeo mabaya ya Mechi zao za kwanza walizocheza Ugenini.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates