Pages

Sunday, 1 March 2015

AZAM YAFUMULIWA 3-0 NA EL MERIKH YATUPWA NJE, KMKM NAO NJE, POLISI MATUMAINI MADOGO LEO YANGA MWENDO MDUNDO

AZAM FC Usiku huu wametandikwa Bao 3-0 na El Merreikh ya Sudan na kutupwa nje ya CAF CHAMPIONS LIGI kwa Jumla ya Mabao 3-2.
Bao ambalo liliimaliza kabisa Azam FC lilifungwa Dakika za mwisho kabisa na Allan Wanga, Mchezaji kutoka Kenya.
Hadi Haftaimu, Azam FC walikuwa nyuma kwa Bao 1-0 na walipigwa Bao la Pili Dakika ya 85.
Huko Zanzibar, KMKM iliifunga Al Hilal ya Sudan Bao 1-0 lakini wanakwenda nje ya CAF CHAMPIONS LIGI baada ya kupoteza Mechi ya Kwanza Bao 2-0.
Hali hii imeiacha Yanga kuwa pekee Timu ya Tanzania kusonga michuano ya Klabu Afrika baada ya kuibwaga BDF XI ya Botswana Jumala ya Bao 3-2 kufuatia kushinda Mechi ya Kwanza 2-0 na kufungwa ya pili 2-1
Kwenye Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Yanga watacheza na FC Platinum ya Zimbabwe ambayo imeicharaza Sofapaka ya Kenya Bao 2-1 katika kila Mechi ya Mechi zao 2.
Polisi ya Zanzibar itacheza Mechi yake ya Pili ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho hapo Jumapili lakini wana kibarua kigumu kufuzu baada ya kuchapwa 5-0 huko Gabon na FC Mounana.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates