KEPTENI Wayne Rooney jana Uwanjani Old Trafford alipiga Bao 2 na kuiwezesha Manchester United kuishinda Sunderland Bao 2-0 na kukamata Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England.
Hadi Mapumziko, Mechi hii ilikuwa 0-0 lakini kwenye Dakika ya 66 Man United walipewa Penati ambayo pia ilileta utata baada ya Refa Roger East kumtoa Wes Brown badala ya John O’Shea kwa kumchezea Falcao Falo iliyozaa Penati hiyo.
Penati hiyo ilifungwa na Wayne Rooney ambae alipiga Bao la Pili katika Dakika ya 84 kufuatia Shuti la Januzaj kutemwa na Kipa Pantilimon na Rooney kuunganisha kwa Kichwa.
MATOKEO YA MECHI NYINGINE
West Ham 1 Crystal Palace 3
Burnley 0 Swansea 1
Newcastle 1 Aston Villa 0
Stoke 1 Hull 0
West Brom 1 Southampton 0
0 comments:
Post a Comment