Barcelona, wakicheza Ugenini huko Estadio Nuevo Los Carmenes, wameifunga Granada Bao 3-1 katika Mechi ya La Liga.
Bao za Barcelona zilifungwa na Ivan Rakitic, Dakika ya 25, na Luis Suarez, Dakika ya 48 lakini Granada wakapata Bao lao moja kwa Penati ya Dakika 53.
Lionel Messi alipiga msumari wa mwisho Dakika ya 70 na kuwapa Barcelona Bao 3-1 ambao umewafanya wawe Pointi 1 nyuma ya Vinara Real Madrid ambao wanacheza Jumapili wakiwa kwao Santiago Bernabeu na Villareal.
MECHI ZA LEO
Jumapili Machi 1
1400 Valencia C.F v Real Sociedad
1900 SD Eibar v Athletic de Bilbao
2100 Sevilla FC v Atletico de Madrid
2300 Real Madrid CF v Villarreal CF
0 comments:
Post a Comment