Pages

Sunday, 8 March 2015

FA CUP MASHABIKI WAVAMIA UWANJA ASTON VILLA IKITINGA NUSU FAINALI BAADA YA KUIBABUA WBA 2-0 LEO LIVERPOOL NA BLACKBURN ROVERS


Aston Villa imetinga Nusu Fainali ya FA CUP baada ya Jana kuwachapa West Bromwich Albion Bao 2-0 Uwanjani Villa Park.
Bao za Villa kwenye Dabi hii ya Midlands zilifungwa Kipindi cha Pili na Fabian Delph na Scott Sinclair.
WBA walimaliza Mechi hii wakwa Mtu 10 baada ya Claudio Yacob kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano mbili.
Mechi hii ilishuhudia Mashabiki wakivamia Uwanja kabla Filimbi ya mwisho kupigwa na ililazimika watelowe ili Mechi iendelee.
Katika Mechi nyingine ya Robo Fainali, Bradford na Reading zilitoka 0-0.
Hii Leo huko Anfield, Liverpool watacheza na Blackburn Rovers katika Robo Fainali nyingine ya FA CUP, Raundi ambayo itamalizika Jumatatu Usiku huko Old Trafford wakati Man United watakapocheza na Mabingwa Watetezi Arsenal.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates