Pages

Saturday, 7 March 2015

LIGI KUU VODACOM AZAM USHINDI 1-0 DHIDI YA JKT COAST NA KAGERA SARE 2-2

BAO pekee kutoka kwa Mrundi, Didier Kavumbagu limeiwezesha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kulipa kisasi kwa JKT Ruvu.
Azam walipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi na kuifanya timu hiyo kuzidi kuwapumulia Yanga waliopo kileleni ambao leo watashuka dimbani kuvaana na Simba.
Kavumbagu alifunga bao hilo lililokuwa la tisa kwake msimu huu katika ligi hiyo katika dakika ya 17 akiunganisha mpira wa krosi ya beki Shomari Kapombe na yeye kuufungwa kwa kichwa.
Azam imefikisha pointi 30, moja pungufu na ilizonazo Yanga yenye 31 ambao leo watakuwa vitani dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa Kati mechi ya mkondo wa kwanza JKT Ruvu ndiyo iliyokuwa timu ya kwanzsa iliyovunja rekodi ya Azam ya kushinda mechi mfululizo 38 baada ya kuichapa bao 1-0.
Katika mchezo mwingine wakicheza nyumbani mkwakwani Tanga timu ya Coastal Union imeshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya goli 2-2 na Kagera Sugar
Coast walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema dakika ya 10 kupitia kwa Selemani kibuta
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika coast walikuwa mbele kwa bao moja kipindi cha pili kagera sugar walisawazisha dakika ya 53 kupitia kwa Atupele green na lingine dakika ya 83 likifungwa na rashidi Mandawa huku goli la pili la coast likifungwa na Rama Salim dk ya 78

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates