
Hadi sasa Arsenal wameshinda Mechi 8 mfululizo za LIgi, wakiwa ndio Timu pekee Msimu huu kuwa na wimbi refu la ushindi, na sasa wapo Nafasi ya Pili wakiwa POinti 7 nyuma ya Vinara Chelsea wenye Mechi 1 mkononi.
Wenger ameeleza: "Hakuna kilichobadilika. Chelsea wako mbali na hawana karaha. Kwa Ubingwa, tunahitaji tushinde kila Mechi na Chelsea kupoteza. Hilo halipo mikononi mwetu.!"
Kwenye FA CUP, Arsenal, ambao ndio Mabingwa Watetezi, wapo Nusu Fainali na Aprili 18 watacheza Uwanjani Wembley Jijini London na Aston Villa
0 comments:
Post a Comment