Mashabiki wa timu ya mashetani wekundu wamejawa na furaha na starehe kubwa baada ya Manchester United kuwabonda Jirani zao Manchester City Bao 4-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Ushindi huu wa Man United umewachimbia Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Timu ya 2 Arsenal na Pointi 4 mbele ya City ambao wako Nafasi ya 4.
Pia ushindi huu umemaliza uteja wa Man United wa kufungwa Mechi 4 mfululizo katika Dabi ya Manchester na kuhakikisha pia ile historia ya kutofungwa mara 5 mfululizo na Mpinzani yeyote inadumishwa.
MAGOLI YA MAN U 4
-Ashley Young, Dakika ya 14
-Marouane Fellaini 27
-Juan Mata 67
-Chris Smalling 73
MAGOLI YA MAN CITY 2
-Sergio Aguero, Dakika ya 8 na 89
*****************
Kipigo hiki kwa City kimeleta hali tete kabisa kwani ni kipigo chao cha 6 katika Mechi 8 na hii itafanya Meneja wao Manuel Pellegrini kuwa tumbo joto.
0 comments:
Post a Comment