Pages

Sunday, 12 April 2015

YANGA YASOGELEA UBINGWA SHERMAN,TELELA NA CANAVARO WATUPIA 3-1 DHIDI YA MBEYA CITY

Yanga hii leo waliwakaribisha Mbeya ciy katika uwanja wa Taifa na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1, matokeo yanayo wafanya wakaribie kujihakikishia ubingwa wa Tanzania bara.
Yanga waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 18 kupitia kwa Kpah Sherman ambapo ni goli lake la pili katika ligi kuu ya vodacom.
Kuingia kwa goli hilo lilipelekea Mbeya city nao kujaribu kupeleka mashambulizi ambapo walifanikiwa kutengeneza nafasi mbili za kujipatia goli la kusawazisha lakini waliishia kuzipoteza.

Katika dakika ya 38 Yanga waliandika goli la pili kupitia kwa Salum Telela aliyeunga mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima na kuifanya yanga kwenda mapmziko wakiwa na goli 2.
Mbeya city walipata goli lao katika dakika ya 40 kupitia kwa Themi Felix 'Mnyama na kupelekea yanga kuongeza kasi katika kulishambulia lango la Mbeya city bila mafanikio na kupelekea mchezo kwenda mapumziko mbeya City 1 yanga 2



 Yanga walirejea kipindi cha pili kama walivyomaliza kipindi cha kwanza na katika dakika ya 51 mpira wa faulo uliopigwa na Haruna Niyonzima uliungwa vyema na nahodha Nadir Haroub Cannavaro na kuipatia goli la 3 yanga sc.

Katika dakika ya 56 mshambuliaji wa Mbeya city Themi Felixs alizawadiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumkwatua Salim Telela, na kupelekea Mbeya ity kumaliza wakiwa pungufu.

Baada ya kadi hiyo nyekundu Telela alitolewa nnje na nafsi yake kuchukuliwa na Said Dilunga huku Mbeya city wakifanya mabadiliko ya wachezaji wa wili waliopelekea kupunguza kasi ya yanga.
Mpaka mwamuzi wa mchezo huo Akrama akipuliza kipenga cha mwisho, Yanga walikuwa mbele kwa goli 3 dhidi ya goli 1 a Mbeya city.

Kwa matokeo hayo yanga wanazidisha wigo wa tofauti ya poinyi baina yake na Azam Fc kutoka katika pointi 5 mpaka kufikia pointi 8.
MSIMAMO LIGI KUU BARA

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates